Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Blinken amaliza ziara ya nchi nne za Afrika

 Blinken Amaliza Ziara Ya Nchi Nne Za Afrika Blinken amaliza ziara ya nchi nne za Afrika

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: Voa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameyapongeza maendeleo ya ujenzi wa njia ya Lobito, kiungo muhimu cha reli cha kusafirisha nje nje vyuma kutoka katikati ya ukanda wa shaba barani Afrika, wakati wa ziara nchini Angola siku ya Alhamisi.

Marekani imekuwa ikiuunga mkono mradi huo unauiunganisha nchi hiyo yenye utajiri wa madini ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia hadi bandari ya Lobito nchini Angola ili kukwepa msongamano wa usafiri huko Afrika ambao umekua ukikwamisha usafirishaji nje wa shaba na Cobalt.

“Leo nilipata fursa ya kuona baadhi ya maendeleo makubwa ambayo tayari yameijenga njia hii. Inasonga mbele zaidi na kwa kasi, nafikiri hicho ndicho tunachofikiria” Blinken aliuambia mkutano wa waandishi wa habari, akiwa pamoja na waziri mwenzake wa Angola Tete Antonio.

Marekani imedhamiria kufadhili ukarabati wa kilometa 1,300 wa reli iliyopo na kuchukua hatua ya kwanza ya kujenga kilometa nyingine 800” aliongeza.

Blinken alisema upanuzi wa njia hiyo utaweza kuhakikiasha usafirishaji wa madini nyeti na kuchochea uwekezaji katika mawasiliano, kilimo, na sekta nyingine.

Blinken alizisifu juhudi za Rais wa Angola Joao Lourenco za kupunguza mvutano kati ya Rwanda na DRC na kusema kuwa amezungumza na Lourenco kuhusu jinsi za “kusogeza mbele juhudi za kidiplomasia.”

Blinken amekamilisha ziara yake ya nchi nne za Afrika huko Angola ziara ambayo imempeleka Cape Verde, Ivory Coast na Nigeria. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujadili ushirikiano wa kibiashara, mabadiliko ya hali ya hewa, mioundombinu, afya na usalama.

Chanzo: Voa