Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa Zuma kuolewa na mfalme Mswati

Binti Wa Zuma Kuolewa Na Mfalme Mswati 'kwa Mapenzi'.png Binti wa Zuma kuolewa na mfalme Mswati

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Binti mwenye umri wa miaka 21 wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaolewa na mfalme wa Eswatini , msemaji wa utawala wa mwisho kabisa wa kifalme barani Afrika ameiambia BBC.

Uchumba wa Nomcebo Zuma na Mfalme Mswati wa Tatu ulifanyika rasmi mapema wiki hii mwishoni mwa sherehe ya siku nane ya densi ya mwanzi, ibada ya kitamaduni ya wasichana inayofanyika kila mwaka.

Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 56 kwa sasa yuko katika mpango wa mitala na wake 11 na ameoa mara 15 kwa jumla.

Msemaji wa Eswatini Alpheous Nxumalo alipuuzilia mbali pendekezo kwamba ndoa hiyo itakuwa muungano wa kisiasa.

Bw Zuma, ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini kuanzia 2009 hadi 2018, na Mfalme Mswati tayari ni jamaa kupitia ndoa.

Wakosoaji wanamtuhumu Mfalme Mswati, ambaye anatawala kwa amri na amekuwa kwenye kiti cha enzi kwa miaka 38, kwa kuishi maisha ya anasa na nyumba yake yenye wake wengi, huku wengi wa watu wake wakitaabika katika umaskini.

Eswatini, ambayo hapo awali ilijulikana kama Swaziland, ina wakazi milioni 1.1 na mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya VVU.

Chanzo: Bbc