Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa Ruto aibua gumzo kupewa ofisi Serikalini

Mtoto Wa Rais Binti wa Ruto aibua gumzo kupewa ofisi Serikalini

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Wakenya mtandaoni wanaelezea kutoamini macho yao baada ya kusikia kuhusu kuwepo kwa afisi ya binti wa rais yenye kuhusishwa na binti wa pili wa Rais William Ruto.

Katika video inayosambazwa sana mtandaoni, Charlene Ruto anaonekana akizungumza na hadhira katika mkutano wa kilele nchini Tanzania ambapo anatambulisha “timu yake kutoka Kenya” ikiwa ni pamoja na mshauri wake na mwingine ambaye ni ” mkuu wa biashara na uwekezaji katika ofisi ya binti wa rais”.

Waliohudhuria wanaonekana kujibu kwa sauti kubwa kwa kupiga makofi na baadhi ya vicheko.

“Sielewi kinachochekesha,” Bi Ruto anajibu huku akijaribu kuendelea na utangulizi.

Sheria za Kenya hazina ofisi ya binti wa rais na hakujakuwa na tangazo lolote la umma la kuanzishwa kwa ofisi kama hiyo.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakikashifu kile ambacho wengine wanakiona kuwa matumizi mabaya ya pesa za walipa ushuru.

‘’Charlene Ruto akitambulisha timu yake kutoka ofisi ya binti wa rais ambaye hulipwa kwa pesa za walipa kodi licha ya kuwa ofisi isiyo halali,’’ Mkenya mmoja kwenye Twitter asema.

Mwingine anauliza jinsi ofisi hiyo ilivyoanzishwa na kushirikisha video hii:Wakenya mtandaoni wanaelezea kutoamini macho yao baada ya kusikia kuhusu kuwepo kwa afisi ya binti wa rais yenye kuhusishwa na binti wa pili wa Rais William Ruto.

Katika video inayosambazwa sana mtandaoni, Charlene Ruto anaonekana akizungumza na hadhira katika mkutano wa kilele nchini Tanzania ambapo anatambulisha “timu yake kutoka Kenya” ikiwa ni pamoja na mshauri wake na mwingine ambaye ni ” mkuu wa biashara na uwekezaji katika ofisi ya binti wa rais”.

Waliohudhuria wanaonekana kujibu kwa sauti kubwa kwa kupiga makofi na baadhi ya vicheko.

“Sielewi kinachochekesha,” Bi Ruto anajibu huku akijaribu kuendelea na utangulizi.

Sheria za Kenya hazina ofisi ya binti wa rais na hakujakuwa na tangazo lolote la umma la kuanzishwa kwa ofisi kama hiyo.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakikashifu kile ambacho wengine wanakiona kuwa matumizi mabaya ya pesa za walipa ushuru.

‘’Charlene Ruto akitambulisha timu yake kutoka ofisi ya binti wa rais ambaye hulipwa kwa pesa za walipa kodi licha ya kuwa ofisi isiyo halali,’’ Mkenya mmoja kwenye Twitter asema.

Mwingine anauliza jinsi ofisi hiyo ilivyoanzishwa na kushirikisha video hii:

Chanzo: Bbc