Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa Rais Dos Santos azidi kubanwa

92650 Pic+angola Binti wa Rais Dos Santos azidi kubanwa

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Luanda, Angola. Benki ya EuroBic ya nchini Angola, imetangaza kusitisha uhusiano wake na mwanamke tajiri barani Afrika, Isabel dos Santos.

Isabela ambaye ni binti wa Rais wa zamani wa Angola, Jose dos Santos hivi karibuni alitajwa kuwa mwanamke tajiri barani Afrika. Hata hivyo mwanamke huyo ameingia katika kashfa baada ya kutuhumiwa kupata mali hizo kwa njia ya ufisadi.

Taarifa ya benki hiyo ilisema kuwa bodi ya wakurugenzi katika mkutano wake wa Jumatatu iliyopita imeamua kufuta uhusiano wake wa kibiashara uliyokuwanao na kampuni ambazo mwanamke huyo ana hisa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, benki hiyo pia itachunguza uhamisho wa mamilioni ya fedha yaliyofanywa na Isabela.

Bilionea huyo anamiliki asilimia 42.5 za hisa za EuroBic kupitia kampuni mbili na kumfanya kuwa mwanahisa mkuu wa benki hiyo.

Hata hivyo, mwaka 2017 miezi miwili baadaye baada ya baba yake kustaafu urais binti huyo alifutwa kazi ya uenyekiti wa kampuni ya mafuta nchini Angola.

Pia Soma

Advertisement
Inadaiwa kwamba wakati alipoondoka Sonangol ambayo ni kampuni ya mafuta ya Angola, binti huyo aliidhinisha malipo ya dola 58 milioni.

Kwa mujibu wa Gazeti la The New York Times, binti huyo wa rais alipata mamilioni ya fedha baada ya kufilisi akaunti ya kampuni ya Sonangol katika benki hiyo ya EuroBic.

Hati zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinaonyesha jinsi mwanamke huyo tajiri barani Afrika alivyojipatia mali yake inayodaiwa kuwa na thamani ya dola za Marekani bilioni mbili kwa njia ya ufisadi akiwa nchini kwake.

Tayari serikali ya Angola imetangaza uchunguzi kuhusiana na madai ya ufisadi wa mwakamke huyo.

Vilevile, mali za binti huyo zilizopo nchini Angola zimekamatwa na kumtaka kurejea nchini haraka ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo, Isabaela mwenyewe amekana kuhusika na ufisadi huo akisema kuwa  madai dhidi yake ni ya uongo na kwamba yanashinikizwa kisiasa na Serikali ya Angola

Chanzo: mwananchi.co.tz