Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti wa Mandela, Zindzi Mandela alikuwa na Corona, kuzikwa leo

Zinz 660x400 Binti wa mwisho wa hayati Nelson Mandela

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Binti wa mwisho wa hayati Nelson Mandela, Zindzi Mandela aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini mapema wiki hii alikuwa na maambukizi ya virusi vya corona, Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini SAB imeripoti taarifa hiyo.

Mtoto wa Zindzi, Zondwa Mandela amethibitishakuwa ni kweli mama yake alikutwa na COVID19, amesema hawajui alipopata ugonjwa huo na familia yake inasubiri ripoti ya uchunguzi

Zindzi ambaye ni mtoto wa 6 wa Mandela alikuwa Balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark, anatarajiwa kuzikwa baadae leo.

Chanzo: millardayo.com