Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea Afrika Kusini ampiku Dangote kwa Utajiri

Rupert Bilionea Afrika Kusini ampiku Dangote kwa Utajiri

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti za Bloomberg, Bilionea wa Afrika Kusini Johann Rupert amempita Mfanyabiashara wa Nigeria Aliko Dangote na kuwa tajiri anayeongoza barani Afrika.

Rupert ni Mmiliki wa Kampuni ya Richemont, moja ya Kampuni kubwa duniani inayojihusisha na bidhaa za kifahari, ambayo inamiliki chapa kama Cartier na Montblanc.

Thamani ya Bilionea huyo imefikia Dola za Kimarekani Bilioni 14.3 na kumfanya ashike nafasi ya 147 kwa utajiri duniani, nafasi 12 mbele ya Dangote.

Kushuka kwa utajiri wa Dangote kunaonyesha changamoto za Mazingira ya kiuchumi nchini Nigeria ambapo sehemu kubwa ya shughuli zake hufanyika.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Bola Tinubu wa Nigeria, kumekuwepo na mabadiliko kadhaa ya kiuchumi nchini humo ikiwemo kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta, hali ambayo imesababisha mfumuko mkubwa wa bei.

Kushuka kwa thamani ya Naira kumeathiri kwa kiasi kikubwa utajiri wa Dangote, ambaye alifanikiwa kukuza thamani yake kupitia viwanda vya saruji na sukari, na mwaka jana alifungua kiwanda cha kusafisha mafuta jijini Lagos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live