Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bili yazua balaa, askari akidaiwa kumuua muhudumu wa baa

Article3 Decibel Japanese Sake Bar East Village NYC Bili yazua balaa, askari akidaiwa kumuua muhudumu wa baa

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari mwenye cheo cha Konstebo, Nicholas Masau anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mhudumu wa baa na kujeruhi wengine watatu.

Tukio hilo limetoka jana Jumatano huko Nakuru nchini Kenya ambapo ofisa huyo alizua kizaazaa baada ya kukataa kulipa katika baa ya Vegas alipoletewa bili ya Ksh16000 sawa na (Sh 261,107) kwa pesa za Tanzania.

Tovuti ya Tuko imesema askari huyo alitimua mbio baada ya kufyatua risasi iliyomuua muhudumu huyo na kujeruhi wengine ambao kwa sasa wamelazwa hospitali kwa matibabu.

“Alizua ugomvi na wahudumu wa baa hiyo kutokana na bili za vinywaji alivyokuwa amekunywa, hali ya sintofahamu ilitokea ambapo ofisa huyo akamfyatulia risasi mhudumu wa baa ambaye ni Ann Maina,” ripoti imesema.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Nakuru, Samuel Ndanyi amesema Masau alikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kaptebwa ambapo bastola yenye risasi mbili imepatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live