Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila CHANJO ni marufuku kukusanyika Rwanda, walimu, wanafunzi lazima kuchanja

Rw Bila CHANJO ni marufuku kukusanyika Rwanda, walimu, wanafunzi lazima kuchanja

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasafiri wanaotarajiwa kuingia nchini Rwanda kuanzia sasa hawatokaa siku 14 za karantini na badala yake watatakiwa kuwa na vyeti vinavyoonesha majibu ya vipimo (PCR) wakiwa salama bila maambukizi yoyote.

Serikali ya Rwanda imeamua kufungua uchumi wake rasmi kuanzia October 14, 2021 baada ya idadi kubwa ya wananchi wake kupata chanjo ya COVID-19 huku idadi ya maambukizi mapya ikipungua kwa kasi kubwa.

Zaidi ya chanjo milioni 11 zimesambazwa nchini humo. Taarifa mpya ya Rais Kagame baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri Jumatano ya wiki hii imetoa masharti mapya ya namna ya kukabiliana na maambukizi.

Masharti yaliyolegezwa ni pamoja na maeneo ya biashara kuongezewa muda saa moja kabla ya kufungwa, na ni lazima kuwa na uthibitisho wa kupata chanjo ili kuingia kwenye jiji la Kigali au kufanya mikusanyiko.

Kuanzia October 14, 2021 mikusanyiko yote, vyuo na maofisi haitoruhusiwa kuingia bila kuwa na cheti cha chanjo. Walimu na wanafunzi wote wanalazimika kupata chanjo ili kuweza kuingia maeneo ya vyuo tangu mwaka mpya wa masomo uanze October 10.

Ndani ya siku 4 tu Rwanda imefanikiwa kutoa chanjo kwa watu 500,000 baada ya kutangazwa kwa masharti mapya.

Rwanda inatarajia kutoa chanjo kwa watu milioni 4 hadi kufikia mwisho wa mwaka huu, na chanjo milioni 7.8 hadi kufikia June 2022. Mpaka sasa zadi ya watu milioni 2.7 wameshapata chanjo kamili.

Mpaka sasa Rwanda ina maambukizi ya 1.1% huku maambukizi yakiwa ni watu 98,925 na vifo 1,318 tangu nchi hiyo iliporipoti mgonjwa wa kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live