Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi mwenye umri wa miaka 90 ambaye hukimbia mbio za marathon za kilomita 10

Fbd9f7ea8aad0035 Bibi mwenye umri wa miaka 90 ambaye hukimbia mbio za marathon za kilomita 10

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Christine Beard alikuwa amezoea kutembea hadi wakati jirani yake alipomtambulisha katika mbio za marathon na hajawahi kurudi nyumaTangu alipokuwa na umri wa miaka 58, Beard amekuwa akishindana kwenye mbio za kilomita 10 za marathon kwa miaka 32 na bado ana matumaini ya kuendeleaKulingana na bibi huyo, kando na riadha kumfanya kuwa fiti, pia inamsaidia kufanya shughuli zake za nyumbani bila kusaidiwa

Kwa Christine Beard, mwenye umri wa miaka 90, kushiriki katika mbio za marathon ni kama uraibu wake.

Bibi huyo ambaye ni manusura wa saratani ya matiti, alijitosa kwenye mbio za marathon akiwa na umri wa miaka 58.

Hii ni baada ya jirani yake kumtia moyo kuwa mkimbiaji badala ya kuzoea tu kutembea.

"Nilikuwa muoga sana. Nilikaza viatu vyangu sana. Nilifikiri vitatoka mguuni na mume wangu alijua nitaishia kufanyiwa huduma ya kwanza," aliambia TODAY.

Read also

Dada Aduwaza Wageni kwa Kuhudhuria Sherehe yake ya Bathdei Ndani ya Jeneza

Mbio zamsaidia kuwa fitiKile kilianza kama wasiwasi, kimeguaka kuwa mtindo wake wa maisha kila mwaka akishindana katka mbio kwa miaka 32 sasa.

Alisema kuwa kukimbia kunamsaidia kunyorosha viungo vyake vyote vya mwili na kumuwezesha kusonga haraka.

Kulingana na msafiri huyo, ice cream na matumaini ndio baadhi ya siri zake kuwa buheri wa afya na kuishi maisha marefu.

Ana lengo la kukimbiaBeard alifichua kuwa kando na kukimbia ili kuwa fiti, pia anakimbia kwa sababu ya mume wake ambaye hana uwezo wa kukimbia kutokana na matatizo ya moyo, binti yake ambaye aliangamizwa na saratani ya ubongo na marehemu rafiki yake.

Ajuza huyo alisema kuwa na watu hao akilini akikimbia humtia nguvu ya kuendelea.

Kando na riadha kumfanya kuwa fiti, pia inamsaidia kufanya shughuli zake za nyumbani bila kusaidiwa

Kufikia sasa Beard amezuru mataifa yote ulimwenguni jambo linamfanya kuwa tayari kila mara kujiandaa kukimbia barabarani kwa dakika 15.

Kando na riadha na kusafiri, Beard pia anapenda kusoma na kujitolea kanisani.



Read also

Wakazi Kiambaa Watafuna Minofu ya Rais Uhuru na naibu wake Ruto

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke