Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara zafungwa katikati mwa jiji la Nairobi

Biashara Zafungwa Katikati Mwa Jiji La Nairobi Biashara zafungwa katikati mwa jiji la Nairobi

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: bbc

Biashara zimefungwa katikati mwa jiji la Nairobi huku polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wa upinzani Jumatatu asubuhi.

Kuna mapigano yanayoendelea kwenye barabara kuu ya Kenyatta kati ya polisi na waandamanaji, baadhi yao wakiwarushia mawe maafisa hao wa usalama.

Biashara zimefungwa huku sintofahamu ikitawala katika mji mkuu.

Viongozi wa upinzani wametaka kuwaongoza wafuasi wao hadi ikulu kuandamana dhidi ya kile wanachokiita serikali haramu na gharama kubwa ya maisha.

Polisi pia wamekuwa wakiwakusanya watu katikati mwa jiji.

Inaonekana lengo ni kuzuia waandamanaji kukusanyika.

Chanzo: bbc
Related Articles: