Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ya ubani ilivyogeuka uti wa mgongo Sudani Kusini

Biashara Ubani Ubani Biashara ya ubani ilivyogeuka uti wa mgongo Sudani Kusini

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Sudan Kusini inatategemea kukusanya mapato makubwa ya bidhaa zisizo za mafuta na kugeuza bidhaa hizo kuwa msingi mkuu wa kuendeshea uchumi wake. Inavyoonekana ni kuwa, Juba imeamua kuelekeza nguvu zake kwenye sekta kama ya kusafirisha nje ubani wenye thamani kubwa maarufu kwa jina la Gum Arabic, matunda na mboga mboga kuendeshea uchumi wake badala ya mafuta.

William Anyuon Kuol, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan Kusini amesema hayo katika mji wa Nimule unaopakana na Uganda na kuongeza kuwa, chini ya Mkakati Mpya wa Taifa wa Uwekezaji, nchi yake imegundua kuwa ubani huo ni bidhaa muhimu ya kuiwezesha Sudan Kusini kupata pesa za kigeni kama nchi na kuzidisha vyanzo vyake vya mapato.

Sudan Kusini, ambayo inategemea mapato ya mafuta kwa asilimia 95 kufadhili bajeti yake ya kila mwaka ya fedha, hivi sasa ina mgogoro wa kusafirisha mafuta yake ghafi kupitia Bandari ya Sudan kutokana na vita baina ya majenerali wa kijeshi vinavyoendelea katika ardhi za jirani yake huyo wa kaskazini. Ubani wa aina hii una matumizi mengi duniani

Waziri Anyuon ameongeza kuwa, wameanzisha mpango maalumu ambao uutaimazimisha Benki Kuu ya nchi hiyoi kununua ubani huo kutoka kwa wazalishaji wa ndani na baadaye kuutafutia masoko ya nje ili kupata fedha za kigeni na kusaidia kwenye juhudi za kuleta utulivu wa kiuchumi nchini humo.

Ubani wa Kiarabu au Gum Arabic unapatikana kwenye vigogo vya matawi ya miti ya mshita. Unayeyuka haraka katika maji na chakula na unatumiwa na watu wengi kwa malengo tofauti yakiwemo matibabu, chakula na vinywaji baridi. Pia hutumiwa katika uchapishaji, rangi, gundi, vipodozi, na matumizi mbalimbali ya viwandani, ikiwa ni pamoja kudhibiti mnato katika viwanda vya wino na nguo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live