Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ya kucheza na Majeneza misibani Ghana imeajiri Watu 100

Screenshot 2020 09 28 At 08.18.10 660x400.png Biashara ya kucheza na Majeneza misibani Ghana imeajiri Watu 100

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Tumeshazitazama sana video za hawa Jamaa wa Ghana wakicheza na majeneza misibani, fahamu tu kwamba hii ni kampuni rasmi na wanalipwa kufanya hivi na Benjamin ndie Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, alianzisha hizi staili za kucheza ili kuondoa huzuni misibani ambako vilio hutawala zaidi kuliko kusherehekea maisha ya aliyetangulia.

Mteja anapofika kwenye Ofisi yao anapewa album ya picha ili achague staili gani ya mavazi anayoitaka ambapo Benjamin anasema sasa hivi biashara yake imekua kubwa na anapata muda mdogo sana wa kulala kwani tenda ni nyingi na sasa anawaza hata kufungua matawi ya ofisi yake kwenye Nchi nyingine.

Benjamin anasema pia kazi hii imetoa nafasi kubwa ya ajira kwani kwa sasa ameajiri Vijana zaidi ya 100 Nchini Ghana ambapo 95 ni wa kiume na watano ni wa kike, tazama zaidi simulizi yao kwenye hii video hapa chini.

View this post on Instagram

Tumeshazitazama sana video za hawa Jamaa wa Ghana wakicheza na majeneza misibani, fahamu tu kwamba hii ni kampuni rasmi na wanalipwa kufanya hivi na Benjamin ndie Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, alianzisha hizi staili za kucheza ili kuondoa huzuni misibani ambako vilio hutawala zaidi kuliko kusherehekea maisha ya aliyetangulia. Mteja anapofika kwenye Ofisi yao anapewa album ya picha ili achague staili gani ya mavazi anayoitaka ambapo Benjamin anasema sasa hivi biashara yake imekua kubwa na anapata muda mdogo sana wa kulala kwani tenda ni nyingi na sasa anawaza hata kufungua matawi ya ofisi yake kwenye Nchi nyingine. Benjamin anasema pia kazi hii imetoa nafasi kubwa ya ajira kwani kwa sasa ameajiri Vijana zaidi ya 100 Nchini Ghana ambapo 95 ni wa kiume na watano ni wa kike, Je akifungua tawi Tanzania unadhani atapata biashara?

Chanzo: millardayo.com