Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ndogo 750,000 kutafutiwa soko kimataifa

A3dce58883064ff03990b923321f205f.png Biashara ndogo 750,000 kutafutiwa soko kimataifa

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Uwekezaji Uganda (UIA) imeorodhesha biashara ndogo na za kati 750,000 kwa nia ya kuziunganisha na masoko ya kimataifa.

Biashara hizo ambazo zilianza kuorodheshwa Novemba mwaka jana, zitakutanishwa na kampuni za kimataifa zinazoingiza bidhaa nchini.

Aidha, mamlaka hiyo itawasaidia wajasirimali hao kuboresha viwango vya bidhaa zao na vile vile kukuza biashara hizo katika huduma na kufikia kuwili ziwe ziweze kukubalika kimataifa.

Naibu Mkurugenzi wa UIA, Paul Kyalimpa alisema juzi kuwa, kwa kuorodhesha biashara hizo, mamlaka hiyo inataka kuwawezesha wajasirimali wadogo na wakati wafikie ubora na kupata vyeti vya bidhaa zao kuwa vya viwango vya kimataifa.

"Tunawahamasisha kupitia Taasisi ya Utafiti wa Viwanda ya Uganda kufikia viwango fulani ambavyo vinahitajika na kampuni za kimataifa," alisema.

Biashara ndogo na za kati nchini zimekuwa zikikumbwa na changamoto kadhaa, kati ya hizo ni ukosefu wa soko, upatikanaji mdogo wa mitaji na viwango duni vya bidhaa zinazozalishwa.

Kyalimpa alisema biashara hizo zinatakiwa kukuzwa ili kuwa biashara kubwa kwasababu zinachangia asilimia 80 ya uchumi wa Uganda.

Chanzo: www.habarileo.co.tz