Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bi harusi akamatwa na polisi siku ya harusi

Screenshot 20220824 095140 Google Bi harusi akamatwa na polisi siku ya harusi

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Uganda Wikiendi iliyopita, polisi nchini humo walimtia nguvuni bibi harusi katika siku ya tukio lake kubwa huku video iliyosambazwa mitandaoni ikivutia maoni kinzani kutokana na jinsi polisi hao walivyoonekana wakimburuza na kwenda naye.

Katika kujitetea, polisi hao walisema kwamba mwanamke huyo ambaye siku ya tukio alikuwa amepambwa kama bibi harusi mtarajiwa alikuwa ameiba na kutoroka na pesa kutoka sehemu moja alikokuwa akifanya kazi.

Ila tukio hilo la jinsi maafisa wa polisi walimnyanyua juu kwa juu lilizua ghadhabu miongoni mwa wananchi ambao wengi walitaka kupata majibu kutoka wakuu wa polisi nchini humo.

Inadaiwa mwanamke huyo kwa jina Christine Natuhera alikuwa ametoroka na kiasi cha shilingi milioni 8 za Uganda sawa na shilingi milioni 4 na laki nane za Tanzania kutoka taasis moja ya kifedha alikokuwa akihudumu kama mfanyikazi.

Mwanamke huyo baada ya kukamatwa Jumamosi katika harusi yake, aliachiliwa Jumapili baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rwizi kuamrisha kuachiliwa kwake mara moja bila shruti la aina yoyote ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live