Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Kilimo kuanzishwa Uganda

617a86f378681ed4274b363c7bf19ba3.png Benki ya Kilimo kuanzishwa Uganda

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPALA

SERIKALI inatarajia kuanzisha benki ya kilimo ili kuhakikisha wakulima wanapata mitaji nafuu tofauti na benki za kibiashara.

Rais Yoweri Museveni alisema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa nchi hiyo.

Alisema wanafikiria kuanzisha benki hiyo kutokana na benki za biashara kutoa zaidi mitaji kwa wafanyabiashara wanaoenda China na kuingiza bidhaa na kuuza kwa haraka na kupata fedha.

“Tunataka ufadhili ambao utawapa watu wetu muda wa kutosha kurejesha mikopo, Benki ya Maendeleo ya Uganda iko pale tulikataa kuibinafsisha, lakini pia tunaweza kuanzisha benki ya wakulima ambayo itawapa mitaji nafuu,” alisema.

“Tunataka kuanzisha benki hiyo ili wakulima waweze kuondokana na riba kubwa katika benki za biashara na serikali imeongeza mtaji katika Benki ya Maendeleo Uganda (UDB) katika mwaka huu wa fedha kuwa Sh trilioni 1.1,” alisema.

Rais Museveni alisema changamoto nyingine inayokabili nchi hiyo ni gharama kubwa za umeme na kwamba serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Karuma litakaloongeza uzalishaji wa nishati hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz