Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Equity yakanusha madai kuwa DP Ruto aliwapigia simu kutoa mkopo wa 15B

0d09a64f75e74563 Benki ya Equity yakanusha madai kuwa DP Ruto aliwapigia simu kutoa mkopo wa 15B

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Benki ya Equity imekanusha ripoti kuwa ilitoa mkopo wa KSh 15b kwa mwekezaji baada ya kupokea simu kutoka kwa Naibu Rais William Ruto.

DP Ruto kwenye mahojiano na runinga ya Inooro alisema alipiga simu Equity na rafikiye akapokea mkopo huo.

Equity ilisema haina rekodi zozote za mteja anayejulikana kama Harun Aydin wala kuwepo na mkopo kwakeKamati ya Fedha na mipango ilikuwa imeita uongozi wa benki hiyo ili kutoa ufafanuzi kuhusu kutoa mkopo kwa mwekezaji huyo.

Benki hiyo ilisemahayo wakati wa mahojiano na kamati ya bunge ambapo meneja mtendaji Gerald Warui alifika kwa niaba ya mkurugenzi James Mwangi.

Kamati ya Fedha na Mipango ilikuwa imemuita Mwangi kufika mbele yake ili kufafanua kuhusu ripoti za kutoa mkopo huo kwa Harun Aydin.

"Harun Aydin hana akaunti wala uhusiano wowote na sisi na hatujampa mkopo wowote kama benki ya Equity," Warui alisema.

Suala la mkopo huo liliibuka baada ya Naibu Rais William Ruto kusema alimsaidia mwekezaji huyo kupata mkopo ili kuenda kuwekeza Uganda.



“Wakati nilikuwa Uganda kama mwezi mmoja uliopita, Rais Museveni alinialika kufungua kampuni ya madawa ya kukabili Covid-19. Alinialika kwa sababu mwekezaji ambaye ameanzisha kampuni hiyo alikuja hapa kwa afisi yangu miaka miwili imepita na akaniuliza nimuunganishe na benki ya Equity ili apate mkopo," alisema Ruto.



Alisema alipiga simu kwenye benki hiyo na kumsaidia kupata mkopo huo wa mabilioni ya fedha.

"Nilichukua simu na kupiga Equity na nikawaambia wamsaidia. Aifaulu na kupokea mkopo wa bilioni 15 ambazo alitumia kuenda kuanzisha kiwanda hicho," alisema Ruto.

Benki hiyo hata hivyo imepuuza ripoti hizo huku Warui akisema hana habari zozote kuhusiana na DP kupiga simu katika kampuni.

"Mimi sijui mambo ya mtu kupiga simu, hata hivyo labda nikipata muda wa kutosha naweza kujaribu kujua kama alimpigia yeyote simu kwa sababu tuko na watu wengi wakubwa," alisema Warui.

Swahiba Mturuki wa Ruto Amsukuma Mkuu wa Equity Motoni Kuhusu KSh15B

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke