Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Dunia yasitisha msaada kwa Sudan

Wb Pic Data (600 X 406) Benki ya Dunia yasitisha msaada kwa Sudan

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imesitisha Msaada kwa Sudan baada ya Jeshi la Taifa hilo kufanya Mapinduzi dhidi ya Utawala wa Kiraia mapema wiki hii.

Kusitishwa ghafla kwa Msaada huo kunaweza kuwa na matokeo mabaya kwa Uchumi wa Sudan, wakati huu ambapo unaanza kurejea katika hali yake.

Maamuzi yaliyochukuliwa na Benki ya Dunia na Umoja wa Afrika (AU) dhidi ya Taifa hilo yanaweka shinikizo zaidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi, Jenerali Abdel Fattah Burhan kurejesha Utawala wa Kiraia.

Hatua hii inakuja mara baada ya Jeshi hilo kumuachia huru Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdallah Hamdok aliyewekwa kizuizini Oktoba 25,2021 sambamba na mawaziri wengine wannee na raia mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live