Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Dunia yaivulia kofia Kenya mfumo wa elimu

Elimu Benki Ya Dunia Kenya Benki ya Dunia yaivulia kofia Kenya mfumo wa elimu

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imepongezwa na Benki ya Dunia kwa mageuzi katika mfumo wake wa elimu, ambao umepelekea wanafunzi waweze kuwa na matokeo bora katika masomo ya lugha na hesabu.

Katika ripoti ya uchunguzi ya hivi karibuni, Benki ya Dunia imeonyesha kuboreka kwa kiwango cha kusoma na kuandika au lugha na hesabu ambayo ni masomo mawili ya kimsingi ambayo wanafunzi hukutana nayo mwanzoni mwa masomo yao. Mafanikio hayo yamepatikana pamoja na kuwepo changamoto kama vile msongamano na kuvurugwa ratiba za masomo kutokana na janga la Covid-19.

Miongoni mwa mageuzi ya hivi majuzi katika mfumo wake wa elimu, Kenya inatumia mtaala unaozingatia Ustawishaji Umahiri na Elimu Jumuishi (CBC), ambao unalenga kuangazia elimu ya kivitendo badala ya kusoma kinadharia kwa ajili ya mitihani tu.

Ingawa awali wanafunzi walitumia miaka minane katika shule ya msingi na minne katika sekondari, sasa watatumia miaka sita katika shule ya msingi kisha miaka mitatu katika kile kinachoitwa sekondari ya chini na mitatu zaidi katika sekondari ya juu.

Kenya pia imekumbatia mfumo wa kukuza walimu kitaaluma, kubadilisha mitaala ya mafunzo na leseni ya walimu huku ikisukuma sera ya kitabu kwa kila mwanafunzi na mbinu bora za usimamizi wa shule kwa lengo la kuboresha usalama kwa wanafunzi.

Ripoti ya Benki ya Dunia iliyopewa jina la "Sasisho la Kiuchumi la Kenya: Toleo la 25: Kulenga Juu, Kupata Elimu ili kudumisha ahueni," imesema mabadiliko hayo ndiyo chanzo cha matokeo bora ya kujifunza, na kuwafanya wanafunzi nchini Kenya kufaulu vyema ikilinganishwa na wenzao katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live