Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Dunia yaipa Somalia dola milioni 125 za ukame

Njaa Yaua Watu 50 Nchini Ethiopia Huku Kukiwa Na Ukame Benki ya Dunia yaipa Somalia dola milioni 125 za ukame

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imeidhinisha dola milioni 125 kwa ajili ya kuisaidia Somalia kuanzisha bima ya maafa ya ukame kwa wafugaji 180,000 wakiwemo wanawake 90,000.

Hiyo ni awamu ya kwanza kati ya mbili zinazolenga kuongeza mapato, kuimarisha usimamizi wa madeni na matumizi sahihi ya fedha za umma sambamba na kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi unaozingatia mabadiliko ya hali ya hewa.

Benki ya Dunia imesema kuwa, mpango huo utarahisisha kupewa mikopo midogo midogo makundi ya watu wa kipato cha chini wakiwemo wafugaji ambao wanajishughulisha zaidi katika sekta za uchumi zinazoathiriwa na hali ya hewa kama vile kilimo, uvuvi na biashara ndogo ndogo.

Mpango huo wa DPF pia unataka kupanua upatikanaji wa umeme wa kijani kibichi na wa gharama nafuu, kusaidia maendeleo ya uvuvi kupitia kutumia vyanzo vipya vya ustawi wa uchumi na kuisaidia serikali ya Somalia kugharamia huduma muhimu za umma.

Kuidhinishwa fedha hizo kumekuja wakati Somalia ikiendelea kukabiliwa na misukosuko mingi na inayoingiliana ambayo inazuia ukuaji wa uchumi na inazidisha umaskini.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Somalia imo kwenye orodha ya nchi hatari zaidi duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa huku wataalamu wakitabiri kuweko ongezeko la joto lenye athari mbaya nchini humo.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanazidisha ukali wa ukame na mafuriko ya mara kwa mara nchini Somalia, ambayo yanaingiliana kwa kiasi kikubwa na udhaifu wa kijamii na kisiasa wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live