Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benin yaondoa marufuku ya usafirishaji bidhaa kwenda Niger

Mamia Ya Wanamgambo Wa Jihadi Wafanya Mashambulizi Niger Benin yaondoa marufuku ya usafirishaji bidhaa kwenda Niger

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Benin imeondoa marufuku ya usafirishaji bidhaa kwenda Niger kupitia bandari ya Cotonou. Hayo yametangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa bandari hiyo kufuatia miezi mitano ya vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo iliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.

Jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS iliiwekea Niger vikwazo kufuatia mapinduzi ya Julai 26 yaliyomuondoa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum. Jeshi la Niger liliimtuhumu Bazoum kuwa ni kibaraka wa nchi za kigeni hususan Ufaransa.

Hatua hizo zimepelekea kufungwa mpaka wa Niger na Benin, ambayo imeshuhudia kushuka kwa mapato baada ya usafirishaji wa bidhaa kwenda Niger kupitia bandari zake kusitishwa.

Mkurugenzi Mkuu wa bandari hiyo, Bart Jozef Johan Van Eenoo amesema: "Marufuku inayohusiana na kusimamishwa usafirisha wa bidhaa zilizoagizwa kutoka nje zinazopelekwa Niger katika bandari ya Cotonou imeondolewa."

Hatua hiyo imechukuliwa takriban wiki moja baada ya Rais wa Benin, Patrice Talon kutoa wito wa kuanzishwa upya haraka kati ya nchi yake na nchi jirani ya Niger.

Nchi zote mbili pia zina wasiwasi kuhusu bomba kubwa la mafuta ambalo litairuhusu Niger, moja ya nchi maskini zaidi duniani, kuuza mafuta ghafi katika soko la kimataifa kwa mara ya kwanza, kupitia bandari ya Seme nchini Benin.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live