Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya mafuta yashuka nchini Kenya

Bei Ya Mafuta Yashuka Nchini Kenya Bei ya mafuta yashuka nchini Kenya

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Nishati nchini Kenya (EPRA) imetangaza kupunguza bei za Petroli, Dizeli, na Mafuta ya Taa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Alhamisi, bei ya Petrol itapungua kwa Ksh.7.21, Dizeli kwa Ksh.5.09 na Mafuta ya Taa kwa Ksh.4.49.

Kufuatia mpango huo mpya lita moja ya petroli jijini Nairobi itauzwa kwa Ksh.199.15, dizeli kwa Ksh.190.38 na Mafuta ya Taa kwa Ksh.188.74.

Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia saa sita usiku, Machi 15 hadi Aprili 14, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live