Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya chai ya Uganda yashuka

5f14563737ba1f48fef84f140636ba48 Bei ya chai ya Uganda yashuka

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BEI ya chai ya Uganda imeendelea kuwa ya chini ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinauza bidhaa hiyo kupitia mnada wa Mombasa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika Mnada wa Mombasa, chai ya Uganda imeuzwa kwa bei ya chini kuliko ya Kenya, Rwanda na Burundi.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, minada ya Januari 12 na 13 mwaka huu, kilo moja ya chai ya Uganda iliuzwa kwa Sh 4,810 ikiwa ni chini ya Sh 8,806 ya chai Kenya, ambapo Rwanda iliuza kwa kilo moja kwa Sh.11,951 na Burundi Sh 9,139.

Kulingana na utendaji wa kila mwaka wa Benki ya Uganda kwa kipindi kilichoishia Novemba, mwaka jana, serikali ilipata Sh bilioni 311 ambazo ilikuwa chini ya Sh bilioni 322 zilizopatikana katika kipindi kati ya mwaka 2018 na 2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhamasishaji wa Uuzaji Uganda, Elly Twineyo alisema bei ya chai imekuwa chini tangu 2018.

Chai ni moja wapo ya mazao yanayouzwa nje ya Uganda kupitia mnada wa Mombasa.

Chanzo: habarileo.co.tz