Mlipuko ulisababisha vifo vya takriban watu kumi na mmoja kwenye basi katikati mwa nchi ya Mali umetajwa kusababishwa na ghasia za wanajihadi, katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara.
Basi hilo, lilipigwa na kitu kinachohisiwa kuwa ni kilipuzi cha kurushwa na makombora, katika barabara ya Bandiagara na Goundaka, iliyopo eneo la Mopti wakati wa majira ya mchana.
Kiongozi wa Jumuiya ya Vijana ya Bandiagara, Moussa Housseyni amesema “Tumehamisha miili tisa kwenye kliniki na bado haijaisha, ila kwasasa tunataka kufuatilia chanzo cha mauaji haya ya kikatili maana si jambo la kawaida kushambulia raia.”
Afisa wa polisi, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alitoa idadi ya waliokufa kwa muda na wengi kujeruhiwa vibaya, huku majeruhi wakisema Mali inapambana na uasi wa muda mrefu wa wanajihadi ambao umegharimu maisha ya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamia ya maelfu kuyahama makazi yao.
Migodi na vifaa vya vilipuzi vilivyoboreshwa (IEDs), ni miongoni mwa silaha za chaguo la wanajihadi ambao wanaweza kulipua wakati wa athari au kulipuliwa kwa mbali ikiwa wanakabiliwa na ulazima wa kufanya shambulizi ingawa wakati mwingine hufanya hivyo kwa kujihami.
Ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), iligundua kuwa kufikia Agosti 31, 2022 migodi na vifaa vya kutengenezea silaha vilisababisha vifo vya watu 72 wengi wakiwa ni wanajeshi na robo ni raia wa wakaida.