Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi latumbukia mtoni na kuua 9

Ajali 91468 Basi latumbukia mtoni na kuua 9

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu tisa wamethibitishwa kufariki baada ya basi walimokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto Mbagathi uliopo jijini Nairobi, vimeripoti vyombo vya habari nchini nchini humo.

Basi hilo mali ya Naboka Sacco lilikuwa likielekea Nairobi kutoka Gataka, katika mtaa maarufu wa Karen wakati dereva ambaye ni miongoni mwa waliopoteza maisha, aliposhindwa kulimudu gari na kuacha Barabara.

Watu sita walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki walipokuwa wakipatiwa matibabu. Polisi wamesema kuwa dereva alikosa udhibiti wakati breki ya gari ilipokatika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live