Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi la kwanza linalotumia umeme lazinduliwa Nairobi

Basi La Kwanza Linalotumia Umeme Lazinduliwa Nairobi Basi la kwanza linalotumia umeme lazinduliwa Nairobi

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: BBC

Sweden imeanzisha teknolojia ya majaribio ya mabasi ya umeme jijini Nairobi, Kenya.

Kampuni hiyo itatoa huduma ya usafiri kwa muda wa miezi 12 ijayo katika wilaya kuu za kibiashara na pembezoni mwa jiji.

Kwa kuanza, kampuni hiyo ya Roam imezindua basi moja ambalo linaweza kubeba abiria 77.

Litakuwa basi la kwanza linalotumia umeme kufanya kazi jijini Nairobi, jiji lenye zaidi ya watu milioni nne.

Ingawa wanalenga kuleta jumla ya mabasi 100 ndani ya miaka miwili ili kuendeshwa na mtoaji wa huduma za mitaa na mamlaka ya jiji la Nairobi.

Uzinduzi huo unaonekana kama sehemu ya mpango wa serikali ya Kenya kuzindua mfumo wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) katika mji mkuu.

Chanzo: BBC