Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la Usalama latakiwa kutoa tamko kuhusu MONUSCO kuondoka DRC

Vikosi Munucos DRC Baraza la Usalama latakiwa kutoa tamko kuhusu MONUSCO kuondoka DRC

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kutoa kauli yake kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na mwezi Agosti mwaka huu kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuondoka kwa ujumbe wa Umoja huo wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO).

Mwito huo umetolewa na mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bintou Keita na Mkuu wa MONUSCO wakati akihutubia Baraza hilo jijini New York, Marekani lililokutana kujadili hali ya usalama kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu ambako vita mashariki mwa nchi hiyo vimesababisha janga la kibinadamu.

Bi. Keita amesema tayari mamlaka za DRC zimepitisha mpango uliorekebishwa wa kuondoka kwa MONUSCO nchini humo akisema, “hii ni hatua muhimu kuelekea kuongeza kazi ya kuondoka kwa ujumbe huo, huku ukihakikisha mchakaot huo unatekelezwa taratibu lakini kiuwajibikaji.”

Amesisitiza kuwa MONUSCO hivi sasa itashirikiana na mamlaka za DRC kuelekea utekelezaji wa mpango huo, huku ikiendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Baraza la Usalama. Hata hivyo amesema cha kusikitisha MONUSCO inaendelea kulengwa na taarifa potofu na za uongo, pamoja na vitisho vya kushambuliwa huku akishutumu mauaji ya raia yaliyofanywa na vikosi vya taifa vya usalama tarehe 30 mwezi uliopita wa Agosti na kwenye mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini. Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bintou Keita na Mkuu wa MONUSCO

Serikali ya DRC ilipata fursa ya kuzungumza kwenye Baraza hilo kupitia Naibu Waziri wake Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Christophe Lutundula. Yeye amesema mpango wa marekebisho ulioandaliwa kimkakati na serikali ya DRC kuhusu kuondoka kwa MONUSCO unalenga; kuondoa mvutano uongezekao kila uchao kati ya MONUSCO na raia, kuepuka kujirudia kwa matukio ya majonzi yatokanayo na shinikizo la kuondoka kwa vikosi vya UN au kuondoka kwa ghasia.” Akihutubia hivi karibuni katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alisema kuwa, uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC utafanyika kama ilivyopangwa mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 na wakati huo huo tunaomba kutekelezwa kwa ombi letu la kuongeza kasi ya kuondoka kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live