Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la Usalama lataka wanajeshi kuuachilia mji wa El Fasher Sudan

Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Lataka Wanajeshi Kuuachilia Mji Wa El Fasher Sudan Baraza la Usalama lataka wanajeshi kuuachilia mji wa El Fasher Sudan

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limevitaka vikosi vya kijeshi vya Sudan kusitisha mzingiro wao wa wiki nane wa eneo la El Fasher, mji wa jimbo la Darfur ambako mapigano yamezua wasiwasi wa mauaji ya kimbari.

Jeshi la Sudan limekuwa likipigana na Wanajeshi wa RSF kwa zaidi ya mwaka mmoja, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

El Fasher ndio kituo kikuu cha mwisho cha mijini huko Darfur ambacho kimesalia mikononi mwa jeshi la Sudan.Baraza la usalama limetoa wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano" na kuondolewa kwa wanajeshi wote katika jiji hilo.

Baraza hilo lenye wanachama 15 siku ya Alhamisi lilipitisha azimio lililoandaliwa na Uingereza, likiwa na kura 14 za ndio, huku Urusi ikijizuia.Ilionyesha "wasiwasi mkubwa" katika kuenea kwa vurugu na ripoti za kuaminika kwamba RSF inatekeleza "vurugu za kikabila" katika jiji la El Fasher.

Katika taarifa yake, baraza hilo lilitoa wito kwa vikosi vinavyohasimiana "kusitishwa mara moja kwa uhasama, na kutafuta suluhu endelevu kwa mzozo huo, kupitia mazungumzo".

Azimio hilo limezitaka pande zote kuruhusu raia wanaotaka kuondoka El Fasher kufanya hivyo na kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.

Mjumbe wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Barbara Woodward aliliambia baraza hilo kuwa "shambulio dhidi ya jiji litakuwa janga kwa watu milioni 1.5 wanaohifadhi katika jiji hilo"."

Baraza hili limetuma onyo kali kwa wahusika katika mzozo leo. Mgogoro huu wa kikatili na usio wa haki unahitaji kukomeshwa," aliongeza.

Louis Charbonneau wa Human Rights Watch alisema azimio hilo "linaweka Vikosi vya Wanajeshi vya Sudan na Vikosi vya RSF kwenye taarifa kwamba ulimwengu unatazama".

Chanzo: Bbc