Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la Usalama UN kupiga kura kuindolea vikwazi Somalia

Umoja Wa Mataifa Afrika Demo Baraza la Usalama UN kupiga kura kuindolea vikwazi Somalia

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kupiga kura baadae hivi leo kuondoa vikwazo vya silaha kwa nchi ya Somalia, ikiwa ni zaidi ya miaka 30 baada ya marufuku hiyo kuwekwa kwa mara ya kwanza.

Somalia iliwekewa vikwazo mwaka 1992 ili kudhibiti usambazwaji wa silaha kwa wababe wa kivita waliokuwa wakipigana, ambapo walikuwa wamemuondoa madarakani dikteta Mohamed Siad Barre na kuitumbukiza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Baraza hilo linatazamiwa kupitisha maazimio mawili yaliyoandaliwa na Uingereza - moja ni kuondoa vikwazo kamili vya silaha kwa Somalia na lingine kuweka tena vikwazo vya silaha kwa wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al Qaeda.

Aidha katika pendekezo hilo, nchi wanachama zinaitaka Somalia kujenga vituo salama vya kuhifadhia silaha ikiwa ni pamoja na ukarabati wa miundombinu iliyoko.

Serikali ya Somalia kwa muda mrefu imekuwa ikiomba vikwazo hivyo kuondolewa ili iweze kuimarisha vikosi vyake kukabiliana na wanamgambo wa Al Shaabab.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live