Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la Mawaziri wa SADC kufanyika kwa njia ya Mtandao

0a117fd512ed4d5d83310778e9930c8f Baraza la Mawaziri wa SADC kufanyika kwa njia ya Mtandao

Sun, 14 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KIKAO cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC- TROIKA ) kilichofanyika kwa njia ya Mtandao kimeridhia mapendekezo ya Mawaziri wa Afya wa SADC kutaka kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kifanyike kwa njia ya Mtandao ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID 19 katika ukanda wake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , William Ole Nasha aliyeshiriki kikao hicho cha SADC Troika akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema kikao hicho kilikutana kwa ajili ya kupitia na kujadili mapendekezo ya Mawaziri wa Afya wa SADC kilichofanyika Januari 29, 2021.

Alisema Mawaziri wa Afya walipendekeza kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri kifanyike kwa njia ya mtandao na kikao cha Wakuu wa Nchi kilichokuwa kifanyike mwezi Machi kisogezwe mbele na sasa kitafanyika kati ya mwezi Mei au Juni kutegemeana na hali ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 itakavyokuwa na kuongeza kuwa vikao vingine vyote vitafanyika kwa njia ya mtandao hadi hapo hali ya maambukizi itakapokuwa imetengemaa.

Vikao hivyo viwili vilikuwa vifanyike mwezi Machi ana kwa ana nchini Msumbiji.

Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha maofisa waandamizi na Katibu Mkuu Wizara ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge alishiriki kikao hicho ambacho pia kilifanyika kwa njia ya Mtandao.

Chanzo: habarileo.co.tz