Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza Kuu la Waislamu Kenya launga mkono mazungumzo ya kitaifa

Kenya: Ruto Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mawaziri Baraza Kuu la Waislamu Kenya launga mkono mazungumzo ya kitaifa

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza Kuu la Waislamu Nchini Kenya (SUPKEM) limeunga mkono mazungumzo kuhusu masuala ambayo yameibuliwa vijana wanaofanya maandamano dhidi ya serikakli ya Rais William Ruto maarufu kama na Gen Z ili kukomesha zogo la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa nchini humo.

Mwenyekiti wa Supkem, Hassan Ole Naado, amesema kuwa baraza hilo linataka muafaka wa kisiasa ufikiwe ili kuyashughulikia baadhi ya matatizo ambayo yameibuliwa na Gen Z wakati wa maandamano yao.

“Maandamano ya Gen Z yameweka wazi kuwa kuna masuala ambayo yanahitaji utatuzi nchini. Nchi inastahili kuanzisha mazungumzo hayo ili masuala ambayo yaliibuliwa na Gen Z yashughulikiwe kwa ukamilifu,” amesema Bw Ole Naado.

Mwenyekiti wa Supkem ambaye alikuwa akizungumza katika makao makuu ya Supkem jijini Nairobi aliongeza kuwa nchi inaweza kusonga mbele tu kama Gen Z na serikali wataafikiana.

Wakati huo huo, Supkem imejiondoa katika kesi ambayo ililenga kuwaondoa mamlakani Rais William Ruto na Naibu Rais, Rigathi Gachagua.

Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanaharakati Cyprian Nyamwamu, Khelef Khalifa, Janet Muthoni, Paul Rukaria, Fred Ogolla na wenzao sita.

Kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa Alhamisi wiki jana, wahusika waliwataka Rais Ruto na Bw Gachagua wajiondoe mamlakani kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa uongozi bora kwa Wakenya tangu wachaguliwe mnamo 2022.

Walisema kuwa Rais na naibu wake wamekiuka Katiba mara 31 hasa kupitia kuwaongezea Wakenya ushuru maradufu, kuamrisha waandamanaji wauawe, waandamanaji kutoweka katika njia ya kutatanisha, kupanda kwa gharama za maisha na serikali kutia saini mikataba ya kibiashara na Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live