Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara kufungwa kupisha sherehe ya 'birthday' ya mtoto wa Rais

Muhoziiii Sherehe Barabara kufungwa kupisha sherehe ya 'birthday' ya mtoto wa Rais

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Uganda wametangaza kufunga barabara baadhi katika mji wa Kampala siku ya jumamosi ya tarehe 30, Aprili 2022 ili kupisha tafrija ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mtoto wa Rais Museveni anayetimiza miaka 48.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba mtoto wa kwanza wa kiume aliyeshika nafasi ya pili ya amiri jeshi mkuu wa majeshi ya nchi kavu amepanga shughuli mbalimbali za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni pamoja na tafrija itakayofanyika katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval ambapo wanamuziki na viongozi nyota watakuwepo.

Kamanda wa Trafiki Kampala Kauma Rodgers alithibitisha kuwa tafija hiyo inaweza kuleta msongamano mkubwa magari utakao athiri sehemu za mji huo mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live