Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bara la Afrika laazimia kuagiza dawa ya kutibu Corona

AFRIKA COVID Bara la Afrika laazimia kuagiza dawa ya kutibu Corona

Fri, 14 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika linalosimamia afya ya umma barani Afrika linafanya mazungumzo na kampuni ya Pfizer kuhusu bara hilo kuagiza dawa ya kumeza inayoitwa Paxlovid ya kutibu COVID-19.Dawa hiyo ina ufanisi wa karibu asilimia 90.

Shirika linalosimamia afya ya umma barani Afrika linafanya mazungumzo na kampuni ya Pfizer kuhusu bara hilo kuagiza dawa ya kumeza inayoitwa Paxlovid ya kutibu COVID-19.Dawa hiyo ina ufanisi wa karibu asilimia 90. Kwa mujibu wa data kuhusianna na dawa hiyo inayoitwa Paxlovid imebainika kwamba inaweza kuepusha vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19. Mkurugenzi wa vitengo vya kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC, John Nkengasong, amesema kwa sasa wanafanya majadiliano ya karibu na kampuni ya Pfizer ili kuwezesha upatikinaji wa dawa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live