Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi wa Umoja wa Ulaya ashambuliwa nyumbani kwake Khartoum

Balozi Wa Umoja Wa Ulaya Ashambuliwa Nyumbani Kwake Khartoum Balozi wa Umoja wa Ulaya ashambuliwa nyumbani kwake Khartoum

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Sudan, Aidan O'Hara, ameshambuliwa nyumbani kwake mjini Khartoum, ambako kumekuwa na mapigano makali kati ya vikosi vinavyohasimiana.

Mwanadiplomasia kutoka Ireland "hakujeruhiwa sana", Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Micheál Martin amethibitisha.

Bw Martin alielezea shambulio hilo kama "ukiukaji mkubwa wa majukumu ya kuwalinda wanadiplomasia".

Takriban watu 185 wameuawa na zaidi ya 1,800 wamejeruhiwa katika siku tatu za mapigano, kwa mujibu wa UN.

Jiji limeshuhudia mashambulizi ya anga, makombora na milio mikubwa ya silaha ndogo ndogo.

Jeshi na kundi la wanamgambo linaloitwa Rapid Support Forces (RSF) wanadai kudhibiti maeneo muhimu mjini Khartoum, ambapo wakazi wamekuwa wakijikinga na milipuko.

Bw Martin alimtaja balozi huyo kama "mwanadiplomasia bora wa Ireland na Ulaya ambaye anatumikia Umoja wa Ulaya katika mazingira magumu zaidi".

"Tunamshukuru kwa utumishi wake na tunatoa wito wa kusitishwa kwa haraka kwa ghasia nchini Sudan, na kuanzishwa tena kwa mazungumzo," alisema.

Hapo awali, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aliandika kwenye tweeter kwamba usalama wa majengo ya kidiplomasia na wafanyakazi ni "jukumu la msingi" la mamlaka ya Sudan.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya, Nabila Massrali ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wajumbe wa Umoja wa Ulaya hawajaondolewa kutoka Khartoum kufuatia shambulio hilo.

Usalama wa wafanyikazi ndio uliopewa kipaumbele na hatua za usalama zilikuwa zikitathminiwa, aliongeza.

Chanzo: Bbc