Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi wa Uganda nchini Kenya Hassan Galiwango amefariki Nairobi

Balozi Wa Uganda Nchini Kenya Hassan Galiwango Amefariki Nairobi Balozi wa Uganda nchini Kenya Hassan Galiwango amefariki Nairobi

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Balozi wa Uganda nchini Kenya na visiwa vya Seychelles, Dk Hassan Wasswa Galiwango, amefariki dunia jijini Nairobi, Rebecca Kadaga, Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Uganda na Waziri wa Afrika Mashariki, amethibitisha.

Dkt Galiwango aliteuliwa kuwa balozi mnamo Oktoba mwaka 2020 na kuchukua nafasi ya Phibby Otaala, ambaye aliacha kazi hiyo ili kugombea nafasi ya kisiasa katika jimbo lake.Hata hivyo, Bi Otaala alipinga uteuzi wake na kukataa kukabidhi wadhifa huo, akidai kuwa hajaitwa.

Dkt Galiwango baadaye aliwasilisha stakabadhi zake kwa rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta mnamo Machi 3, 2021. Kabla ya kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuu, Dkt Galiwango alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala wa muda mrefu katika sekretarieti ya chama cha The National Resistance Movement (NRM).

Vilevile alikuwa mume wa mbunge wa Uganda Connie Galiwango.

Rambirambi zilianza kumiminika huku raia wengi wa Uganda kwenye Twitter wakimsifu kuwa "afisa aliyejitolea" na kufanya kazi yake yote ili kuhakikisha haki na ustawi wa Waganda nchini Kenya unazingatiwa.

Chanzo: Bbc