Romania imeamua kumrudisha nyumbani Balozi wake wa nchini Kenya baada ya Balozi huyo kuwafananisha Waafrika na nyani.
Dragos Tigau alitamka maneno hayo ya kibaguzi wakati wa Mkutano kwenye jengo la Umoja wa Mataifa jijini Nairobi mnano Aprili 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP Bw.Tigau alisema "Kundi la Waafrika limejiunga nasi" baada ya kuona Nyani nje ya dirisha.
Suala hili lilijaribu kufichwa lakini Alhamisi ya juzi Afisa wa mambo ya Nje wa Kenya Kamau Macharia alilileta hadharani.
Hapo jana, Wanadiplomasia wa Kiafrika walitaka waombwe msamaha wa wazi, na kusisitiza kuwa msamaha wa kimyakimya hautoshi. Leo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Romania imetangaza kuwa imeanza taratibu za kumrudisha Balozi huyo.
"Tumesikitishwa sana na hii hali na tunaomba msamaha kwa wote walioathirika. Tabia zozote au maoni yenye asili ya kibaguzi hayakubaliki. Tunatumaini hii haitoathiri mahusiano yetu na nchi za Afrika".