Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi aibiwa akitembea Barabarani na walinzi wake

Amb Ofra Farhi.png Ofra Farhi

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Israel nchini Zambia, Ofra Farhi ameibiwa wakati akitembea kwenye barabara za jiji kuu la Lusaka mbele ya walinzi wake walioshindwa kuzuia bosi wao kunyang'anywa mali zake.

Ripoti ya jarida la Times of Israel linasema kuwa wezi hao walimvamia Farhi akitembea na kutoweka na simu yake ya mkononi pamoja na paspoti yake ya kidiplomasia.

Kwa mujibu wa Times of Israle, Farhi alikuwa akivuka barabara yenye shughuli nyingi jijini Lusaka, gari liliposimama kand yake na waliokuwa ndani kuvuta begi yake.

Balozi huyo alianguka baada ya begi hiyo kuvutwa, hali hiyo ikimuacha na majeraha madogo. Kiasi cha pesa kisichojulikana kilikuwa katika begi hiyo.

Walinzi wake ambao walikuwa naye kwa wakati huo walishindwa kuzuia wizi huo na Farhi kusisitiza kuwa kisa kama hicho kinaweza kutokea kokote nchini humo.

"Zambia ni salama na yenye amani ajabu," Balozi Farhi alisema.

Waziri wa Zambia kuhusu Masuala ya Kigeni Stanley Kakubo alimpigia simu Farhi kimahakikishia usalama wake. Kanndo na Zambia, Farhi pia huwakilishia Israel katika mataifa ua Zimbabwe na Botswana.

"Kwa mara zaidi ya moja, mabalozi wa Israel duniani kote huhatarisha maisha yao na ya familia zao ili kuhusumia taifa. Wanastahili kushukuriwa kwa hilo," alisema Eli Cohen, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live