Wanajiolojia wamethibitisha kuwa bahari mpya inaundwa barani Afrika ambayo italigawa bara hilo nusu.
Inasemwa kuwa ufa wenye urefu wa maili 35 ulionekana katika jangwa la Ethiopia eneo la Afar mwaka 2005 na pengine ni mwanzo wa bahari mpya kabisa.
Ukurasa wa The Archeologist umeandika kuwa Jarida la Geophysical Research Letters linalotumia data za tetemeko na utokeaji wa nyufa linasema utengano wa bara la Afrika ulianza taratibu takribani miaka milioni 30 iliyopita.
Mataifa 54 barani Afrika yamegawanywa kulingana na wanajiolojia wanaotafiti juu ya tectonics ya sahani za bara hilo. Ufa wa Afrika Mashariki, unaotenganisha nchi za pwani ya mashariki kama Kenya na Tanzania kutoka sehemu kubwa ya bara, unapitia Msumbiji kutoka eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopia.
Utafiti mpya katika jarida la Nature uligundua kuwa vipande viwili vya ardhi vinatengana kwa kiwango cha milimita 7 kwa mwaka. Mataifa kama Zambia na Uganda yatakuwa na pwani zao.
Wanasayansi wanadai kuwa volkano kadhaa ikiwa ni pamoja na Aloo Dalapila na Erra Ale nchini Ethiopia pamoja na Oldonyo lengai nchini Tanzania, zimesaidia katika mchakato wa utafiti huo.