Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu akutwa amekufa gesti na dawa za ARV pembeni

Gesti?fit=700%2C394&ssl=1 Babu akutwa amekufa gesti na dawa za ARV pembeni

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshtuko mkubwa ulikumba mji wa Bondo katika Kaunti ya Siaya siku ya jana Jumanne asubuhi baada ya mwili wa mzee wa miaka 61 kupatikana ndani ya chumba katika moja ya nyumba za wageni mjini humo.

Inaripotiwa kuwa mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya wageni aliupata mwili wa marehemu Nicholas Ogada Ogol ukiwa umelala juu ya kitanda wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake katika nyumba hiyo ya wageni siku ya Jumanne.

Mara moja msimamizi wa nyumba hiyo ya kulala wageni aliripoti tukio hilo la kutatanisha katika Kituo cha Polisi cha Bondo.

Maafisa wa polisi waliofika katika eneo la tukio walibaini kuwa marehemu aliingia katika nyumba hiyo ya wageni siku ya Jumatatu jioni. Hakuwa ameandamana na yeyote wakati huo na alionekana amelewa kiasi, kulingana na ripoti ya polisi.

Hali ya marehemu haikujulikana hadi siku ya Jumanne asubuhi ambapo mmoja wa wahudumu aliyekuwa akifanya usafi alipogundua mwili wake ukiwa umelala kitandani. Hakukuwa na majeraha yoyote yaliyoonekana kwenye mwili wa marehemu.

Takriban tembe 90 za dawa za matibabu ya ugonjwa wa UKIMWI zilipatikana kando ya mwili wa marehemu, mkuu wa polisi kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo alithibitisha.

Mwili wa Ogol baadaye ulipelekwa hospitali ya kaunti ndogo ya Bondo kwa uchunguzi wa maiti huku polisi wakianza uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live