rancis Bor, mzee wa miaka 72 anadaiwa kumuua mjukuu wake wa miaka 23 kwa kutumia mshale huku sababu ikitajwa mjukuu huyo alikwenda kwa babu yake huyo akiwa amelewa.
Tukio hilo limetokea Chepalungu, Kaunti ya Bomet nchini Kenya. Akiwa kwa babu yake marehemu Ezra Chepkwony inaelezwa ulizuka ugomvi kati yao baada ya Chepkwony kumtusi babu yake.
“Alimtusi na kumchokoza babu yake, jambo lililomfanya mzee huyo kushika upinde na mshale wake kwa nia ya kumpiga mjukuu wake.
“Baada ya kukosa kumpiga Chepkwony na mshale huo, babu Bor aliamua kumdunga mjukuu wake moja kwa moja kupitia mshale huo,” imeeleza Citizen Digital.
Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Chepalungu, Phanton Analo aliiambia Citizen kuwa polisi wamemkamata na kuichukua silaha inayodaiwa kutumiwa na babu anayetuhumiwa kuua.
Huku mwili wa marehemu ukihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kapkate.