Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Watoto 151 na wake 16 aapa kuendelea kuoa hadi kifo

926fff0cedae8f34 Baba wa Watoto 151 na wake 16 aapa kuendelea kuoa hadi kifo

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mzee huyo alisema ana mpango wa kuoa mke wa 17 ili amzalie watoto wengine zaidi akiwa na ndoto ya kuzaa watoto 1000 na kuoa wake 100

- Kulingana na mzee huyo, ndoa ya mitala ni mradi ambao aliuanzisha mwaka 1983 na ataendela nao hadi kifo

- Nyandoro alifichua kuwa kazi yake ni kuketi kwenye kivuli na kusubiri chakula na kuwaridhisha wake zake chumbani

Misheck Nyandoro, muumini wa Kanisa la Johanne Marange Apostolic ambaye ni baba wa watoto 151 kutoka kwa wake 16 amesema hatakoma kuzaa.

Nyandoro kutoka Mbire, eneo la Kati mwa Mashonaland nchini Zimbabwe, alisema ana mpango wa kuoa mke wa 17 ili amzalie watoto wengine zaidi, Gazeti la The Herald limeripoti.

Kulingana na mzee huyo, ndoa ya mitala ni mradi ambao aliuanzisha mwaka 1983 na ataendela nao hadi kifo.

"Yangu ni mradi. Huu mradi wa ndoa ya mitala niliuanzisha tangu mwaka 1983 na nitaumaliza na kifo changu. Wakati nitafariki ndio nitakoma kuoa na kuzaa watoto.

“Ninapanga kuoa mke wangu wa 17 msimu huu wa baridi na tayari mipango inashughulikiwa," alisema Nyandoro.

Kulingana na mzee huyo mwenye umri wa miaka 66, mradi huo unazaa matunda kwani hupokea pesa na zawadi kochokocho kutoka kwa watoto wake na wakwe.

“Kutokea kwa watoto wangu wanaofanya kazi na kuzawadiwa pesa kupitia EcoCash, karibu kila siku, watoto wangu 11 wameniweka kwenye sera ya mazishi. Ninapata zawadi kutoka kwa wakaza wanangu."

“Sijakoma kuzaa wala kuoa. Mungu akiniruhusu, nitaoa hadi wake 100 na huenda kuzaa watoto 1000. Ulaya una mpango wa kupunguza idadi ya watu Afrika na ninapinga.Mimi ni mpiganaji wa kitambo na serikali inashuhulikia katro ya watoto wangu. Hkauna shida," aliongeza.

Nyandoro alifichua kuwa kazi yake ni kuketi kwenye kivuli na kusubiri chakula kutoka kwa wake zake 16 ambapo kila mke hupika na yeye huchagua tu chakula kitamu na kutupa kilichopikwa vibaya akidai ni sheria katika boma hilo.

Mzee huyo alijigamba namna ana uwezo wa kuwaridhisha wake zake chumbani ambapo ana ratiba ya kumtembelea kila mke kuwapa haki zao za ndoa.

Alidai kuwa hatumii dawa zozote za kusisimua mapenzi akisisitiza kwamba ana nguvu sawa na kijana wa miaka 18.

Nyandoro pia alisema alioa wake zake kulingana na sheria za kanisa lake na hajawahi kumuoa mwanamke ambaye aliwahi kuolewa ama mwenye umri mdogo.Yeye ndiye huwatongoza warembo ambao anataka kuwaoa bila kuchaguliwa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke