Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Taifa la Zambia Kaunda afariki

E4Fw36jUYAcAaYZ 660x400.jpeg Baba wa Taifa la Zambia Kaunda afariki

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwasisi wa Taifa la Zambia Kenneth Kaunda amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu ya maradhi ya Pneumonia, Kaunda amefariki akiwa na umri wa miaka 97.

Watoto wake wa kiume Panji na Kambarage Kaunda wamethibitisha, siku tatu zilizopita Kaunda alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Kijeshi mjini Lusaka.

Maafisa hata hivyo hawakuweka wazi maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, lakini baadaye yalibainika kuwa ni Pneumonia wakati Taifa hilo la kusini mwa Afrika likishuhudia kuongezeka kwa maambukizi ya maradhi ya COVID-19.

Kaunda alikuwa akichukuliwa kama mmoja ya manusura wa mwisho miongoni mwa kundi la mashujaa wa uhuru barani Afrika, alitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi 1991.

Chanzo: millardayo.com