Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba na mwanaye wafa kwa ajali wakitoka jandoni

Ajali Kenya Gh Baba na mwanaye wafa kwa ajali wakitoka jandoni

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia mbili huko Njoro, katika Kaunti ya Nakuru zimeghubikwa na majonzi kufuatia vifo vya jamaa zao waliofariki katika ajali mbaya ya barabarani eneo la Ndefo iliyosababisha vifo vya watu wanne.

Katika ajali hiyo iliyotokea Ijumaa, Machi 25, Elizabeth Wangare alimpoteza mumewe, Moses Kihara na mwanawe Francis Mwangi, ambaye alikuwa miongoni mwa watahiniwa milioni 1.2 wa Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kenya (KCPE) 2021.

Wangare amesema wawili hao walikuwa wakisafiri kurejea nyumbani wakitokea kwenye hafla ya jandoni wakati mkasa huo ulipotokea. Wangare alisema mwanawe siku zote alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora na alitarajia kusherehekea matokeo yake ambayo yatatangazwa mapema wiki hii.

"Mara ya mwisho nilizungumza na mwanangu ilikuwa wiki mbili zilizopita wakati akielekea kwenye sherehe ya jandoni, tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atafaulu mitihani yake, kujiunga na shule nzuri ya sekondari kama Alliance Boys na baadaye ndoto zake ilikuwa ni kuwa mhandisi," alisema Wangari.

Benedict Wambugu, mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Molo Academy pia alifariki dunia katika ajali hiyo.

Majeruhi wengine wawili, baba na mwanawe walionusurika kwa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya Nakuru Level Five.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live