Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba na mwanawe washtakiwa kwa kumng'ata pua mwanamke

Kulawitiss Baba na mwanawe washtakiwa kwa kumng'ata pua mwanamke

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja mkongwe mwenye umri wa miaka 71 ameshtakiwa sambamba na mvulana wake katika kile mahakama iliambiwa ni wawili hao kushirikiana na kung’ata pua ya mwanamke mmoja.

Kulingana na jarida la Punch nchini Nigeria, Clifford Udouko na mwanawe Ekomen walifikishwa katika Mahakama ya Ota mjini Ogun Jumanne asubuhi kwa madai ya kumng'ata mwanamke mmoja puani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Polisi waliwafungulia mashtaka washtakiwa hao, ambao anwani zao hazikutolewa, la kushambulia, kula njama na uvunjifu wa amani.

Hata hivyo washtakiwa hao walikana shtaka hilo.

Wakili wa Mashtaka, mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa washtakiwa na wengine kwa ujumla, walitenda kosa hilo Juni 5 majira ya saa 4.50 jioni.

Mwendehsa mashtaka alidai kuwa washtakiwa walimshambulia na kumng’oa pua mlalamikaji, Daramola Olawunmi.

Alisema washtakiwa hao pia walijiendesha kwa njia ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa kutumia lugha za kuudhi.

Mwendesha mashtaka huyo alisema kosa hilo linakiuka masharti ya kifungu cha katiba ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Hata hivyo, hakimu alikubali washtakiwa kuachiliwa kwa dhamana ya jumla ya N200,000 ambacho ni shilingi elfu 42 za Kenya, kila mmoja na mdhamini mmoja katika jumla kama hiyo.

Aliamuru kwamba mdhamini lazima awe ndani ya mamlaka ya mahakama na aajiriwe kwa manufaa na ushahidi wa malipo ya ushuru kwa Serikali ya Ogun. Aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 24 kwa ajili ya kusikilizwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live