Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba ataka kumshushia kipigo mahakamani muuaji wa mwanaye

Er4thytuu Baba ataka kumshushia kipigo mahakamani muuaji wa mwanaye

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja nchini Afrika Kusini amerekodiwa akijaribu kumshambulia mshukiwa anayetuhumiwa kumuua binti yake wa miaka minne.

Binti huyo, Bokgabo Poo, alitoweka wiki iliyopita kabla ya kuthibitishwa kufariki.

Ntokozo Zikhali mwenye umri wa miaka 30 ameshtakiwa kwa utekaji nyara, ubakaji na mauaji ya mtoto huyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Haijulikani ikiwa amepata dhamana. Alifika mahakamani leo,Jumatatu, na kesi ilipokuwa karibu kukamilizika kusikilizwa, baba yake msichana huyo aliruka kutoka kwenye kiti chake na kujaribu kumshika.

Baba huyo alisikika akipiga kelele "umemuua binti yangu", kulingana na tovuti ya habari ya Times Live.

Bw Zikhali atarudi mahakamani wiki ijayo kwa ajili ya kusikilizwa kwa dhamana. Vyombo vya habari vimesambaza picha za vurugu zilizotokea katika chumba cha mahakama huku mshukiwa akiongozwa kwa amri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live