Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba aliyetumia miaka mingi kumtafuta muuaji wa bintiye Kenya afariki dunia

Baba Aliyetumia Miaka Mingi Kumtafuta Muuaji Wa Bintiye Kenya Afariki Dunia Baba aliyetumia miaka mingi kumtafuta muuaji wa bintiye Kenya afariki dunia

Wed, 14 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Baba aliyetumia miaka 35 akijaribu kumsaka muuaji wa bintiye baada ya kuuawa nchini Kenya amefariki dunia.

Mwili wa mpiga picha wa wanyamapori Julie Ward, 28, kutoka Bury St Edmunds, Suffolk, uligunduliwa kwenye hifadhi ya Maasai Mara mnamo Septemba 1988.

Hakuna mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa mauaji yake.

John Ward, ambaye alitumia £2m ya pesa zake mwenyewe kuchunguza kesi hiyo, alikufa ndani ya wiki mbili za mkewe Jan.

Wana wao Bob na Tim walisema wataendeleza misheni ya baba yao.

Bob Ward alisema babake, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 89, aliendelea kufuata maelekezo hadi wiki chache zilizopita.

Alisema, pamoja na kaka yake, wataendeleza kazi ya baba yao, na wanapanga kuchapisha kitabu juu ya kesi hiyo na kutengeneza makala.

"Ulimwengu unaweza kuona kile ambacho amekuwa akifanya kwa miaka 35 iliyopita," aliiambia BBC Radio Suffolk.

"Ni hadithi ya kipekee na nadhani watu wanajua tu nusu yake."

, WARD FAMILYCopyright: WARD FAMILY Mabaki ya Julie Ward yaligunduliwa na babakeImage caption: Mabaki ya Julie Ward yaligunduliwa na babake Miss Ward alitoweka kuelekea mwisho wa safari ya upigaji picha akiwa peke yake.

Mara ya mwisho alionekana akiwa hai tarehe 6 Septemba 1988 kabla ya mwili wake uliochomwa na kukatwa vipande vipande kupatikana na babake wiki moja baadaye.

Wakati huo, maafisa wa Kenya walidai kuwa alishambuliwa na wanyama, lakini walikubali kwamba aliuawa baada ya babake kufichua ushahidi zaidi.

Chanzo: Bbc