Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba akamatwa kwa kumkata matiti binti yake

Polisi Jijini Lagos Polisi jijini Lagos

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: BBC Swahili

Polisi jijini Lagos nchini Nigeria wamemkamata mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Banjo kwa madai ya kuyakata matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka 8 kwa kutumia jiwe la moto.

Taarifa ya polisi inasema kuwa baba huyo alitekeleza unyama huo kwa binti yake, kwa sababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha 'chuchu', ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikieleza kuwa yuko mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi.

Taasisi moja ya kutetea haki za Watoto ndiyo ilitoa taarifa hizo katika Kituo cha Polisi, Msemaji wa polisi wa Jimbo la Lagos, DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Mkuu wa taasisi ya kutetea haki za watoto Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, ameiambia BBC kwamba Banjo, anayefahamika kama Panel; "Aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake, Alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake," alisema.

Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

Mama yake msichana huyo alisema kuwa Banjo amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara.

Comrade Ebenezer alisema kuwa alimwambia baba yake msichana huyo kuwa alifanya uhalifu. Kingine cha kushangaza zaidi ni kwamba, baba huyo amekuwa akimuogesha binti yake wa miaka 8 kila siku.

Chanzo: BBC Swahili