Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumbaka mwanaye na kumzalisha mapacha

Gregory Mwatu Munyao Gregory Mwatu Munyao

Tue, 22 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 36 amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka na kumpachika mimba binti yake wa kambo.

Gregory Mwatu Munyao almaarufu kwa jina ka Boniface anadaiwa kutekeleza kitendo hicho katika makazi yao mtaani Kasarani, Nairobi wakati wa presha za janga la Corona ambapo watu walifungiwa.

“Unashtakiwa kuwa kwa tarehe tofauti kati ya Machi 2020 na Juni 18, 2020, eneo la Kasarani Kaunti ya Nairobi, ulimuingilia kwa nguvu kimwili na kumsababishia majereha ya sehemu za siri mtoto wa miaka 13,” sehemu ya mashtaka ilisema.

Hata hivyo, Munyao ambaye alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Milimani mbele ya Hakimu Mkuu Gilbert Shikwe, alikana kumnajisi bintiye wa kambo.

Akiongozwa katika kujitetea baada ya kula kiapo, Munyao alisema kuwa alimwadhibu tu kinyume na mashtaka yanavyodai kuwa alimnajasi.

“Nilimwambia mke wangu kumwonya binti yetu ambaye alikuwa akisoma dasara la saba katika Shule ya Msingi ya Kasarani kwamba akome kufika nyumbani akiwa amechelewa wakati akitoka shuleni,” Munyao alijitetea.

Munyao aliendelea na kuiambia mahakama kuwa alimlipia binti huyo ada ya shule hata wakati akiishi na bibi yake kabla ya kuhamia kwa mama yake Kasarani.

Akitoa ushahidi wake mahakamani, mlalamikaji ambaye tayari amejifungua watoto mapacha, alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akiingia kwa siri chumbani mwake, kumtoa nguo, kumnajisi na kutishia kumuua iwapo angemwambia mama yake.

Hakimu aliambiwa kuwa mimba hiyo iligundulika na mama yake ambaye alikimbia katika duka la dawa lililokuwa karibu na kununua vifaa vya kupima ujauzito.

Baada ya vipimo kusema ni kweli alikuwa mja mzito, binti huyo alimweleza kila kitu mama yake ambaye alimpeleka hospitalini kabla ya kuripoti katika kituo cha polisi cha Karasani. Kesi hiyo itasikizwa mara ya mwisho mnamo Machi 25, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live