Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baadhi ya wafuasi wa Dhehebu ‘tata’ la Shakahola Kenya 'walinyongwa'.

Dhehebu Tata Baadhi ya wafuasi wa Dhehebu ‘tata’ la Shakahola Kenya 'walinyongwa'.

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Bbc

Baadhi ya wahanga wa dhehebu tata linaloendesha shughuli zake katika msitu wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi waliuawa kwa kunyongwa, yameonyesha matokeo ya vipimo vya miili ya baadhi ya watu 110 iliyofukuliwa.

Zoezi la uchunguzi huo lililoongozwa na mchunguzi mkuu wa miili wa serikali Johansen Odour jana katika Hospitali ya Malindi ulionyesha kuwa watoto wawili walikufa baada ya kuzibwa pua na mdomo.

Maafisa wa uchunguzi wa miili jana waliweza kuchunguza miili ya watoto tisa na mwanamke mmoja. Watoto walikuwa na umri wa kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka kumi, kulingana Dkt Odour.

“Kwa ujumla walikuwa na muonekano wa njaa kali…Lakini miili miwili ya watoto ilikuwa na rangi ya bluu kwenye kucha za vidole vyao vya mikono… hali iliyosababishwa inayofahamika kama asphyxiation. Hii inamaanisha kuwa walinyimwa hewa ya oksijeni wakati walipokufa na hii inaweza kuashiria kuwa huenda walinyongwa ,” Dkt Odour alisema wakati alipokuwa akitoa taarifa ya uchunguzi.

Dkt Odour alisema kuwa kazi ya uchunguzi wa miili ilikuwa na changangamoto mwanzoni kwani ilibidi waweke machine zaX-ray kwa ajili ya kukadiria umri wa marehemu.

Matokeo hayo sasa yanaonyesha mauaji, hususan kwa watoto wengi ambao ndio wengi wa waathiriwa wa shughuli za dhehebu tata lililoongozwa na Mchungaji Mackenzie.

Bw Mackenzie anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Malindi pwani ya Kenya.

Chanzo: Bbc