Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Kukutana na Wajane wa Magufuli na Mkapa, Raila amekutana na Rais Samia

89cb42f1c97fc6e4 Baada ya Kukutana na Wajane wa Magufuli na Mkapa, Raila Apokelewa na Rais Suluhu

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga hii leo amekutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo na wamezungumzia masuala ya uboreshaji wa miundombinu ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

Kama ilivyoripitiwa awali na TUKO.co.ke, Raila alizitembelea familia za mafariki wake Hayati Rais John Pombe Magufuli na Benjamin Mkapa. alipokuwa akirejea nchini kutoka Zambia.

Railaa alitua mjini Dar es Salaam saa chache baada ya kuhudhuria hafla ya uapisho wa rais mpya ya Zambia Hakainde Hichilem.

‘’Nimepitia ili kuziijulia hali familia za rafiki zangu rais Benjamin Mkapa na John Magufuli. Nafurahia kukutana na Anna Mkapa na Janeth Magufuli wakiwa katika hali nzuri’’.Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi’’

Kiongozi huyo amekuwa rafiki wa karibu wa viongozi hao wawili waliofariki na hususan John Pombe Magufuli kabla na hata alipokuwa rais wa Tanzania.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke