Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baa la njaa linavyozidi kuitesa Zambia

Zambia Njaa.png Baa la njaa linavyozidi kuitesa Zambia

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zambia imekuwa ikikosa mvua kwa zaidi ya miezi miwili. Athari za mfumo wa hali ya hewa ya El Niño, iliyozidishwa na mabadiliko ya tabianchi. Ukame umeharibu nusu ya mazao.

Leo, nchini Zambia, zaidi ya watoto milioni moja wana njaa, linaonya shirika lisilo la kiserikali la Save The Children, ambalo limekusanya ushuhuda hasa magharibi mwa nchi hiyo. Kulingana na Malama Mwila, meneja wa sera na utetezi wa kikanda wa shirika hili lisilo la kiserikali, Mashariki na Kusini mwa Afrika, ambaye anajibu maswali kutoka kwa Lucile Gimberg, "hii ina maana kwamba kila siku, wanakula mlo mmoja tu kwa siku. Na tena, chakula hiki hakiwezi kuitwa chakula!

"Bila chakula, wanalala"

"Baadhi ya watu," Malama Mwila anaongeza, "hutumia saa nyingi kwenye savanna au msituni kutafuta matunda ya mwituni kula. Vinginevyo, wanakula tunachokiita hapa mashwa. Ni aina ya mizizi ya majini ambayo huchemshwa ili iweze kuliwa. "

“Tunachokiona katika jamii zilizoathirika ni kwamba watoto hawawezi kwenda shule wakiwa na tumboni hama kitu. Hawawezi kuzingatia. Mama mmoja alituambia kwamba anapowatazama watoto wake, anafikiri kwamba ni wagonjwa. Lakini kwa kweli wanahitaji kula tu. Bila chakula, wanalala, ni utaratibu wa asili unapokuwa na njaa,” anahitimisha meneja huyu wa kikanda wa sera na utetezi wa shirika lisilo la kiserikali la Save The Children.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live